Taifa Leo October 11th, 2015

Zamzam tf

Na Anthony Omuya

Japo ana umri mdogo, anao wingi wa busara na bidii masomoni hali ambayo imechangia Zamzam Suleiman kupokea tuzo zaidi ya tatu.

Zamzam 13, ni  mwanafunzi katika shule ya msingi ya lsiolo Little Angels, darasa Ia nane, ambaye alipokea tuzo kwa kuwa mwanafunzi bora nchini  kwa uandishi wa lnsha ya Ki­ ingereza wakati wa kuwatuza washindi katika ukumbi wa Sarit Centre jijini Nairobi, majuzi.

Ametuzwa kuwa mwanafunzi bora, mtiifu na mwenye bidii ya mchwa. Aidha, amepokea tuzo Ia mkurugenzi wa shule Evans Macha ria, am­ baye anamtaja kuwa mwenye bidii na nidhamu ya hali ya juu.

Anao ufasaha wa kuzungumza na kuan­dika, na haya yalijitokeza wakati wa kuwatuza wanafunzi kwa shindano  Ia insha ambazo zilidhaminiwa na kampuni za uchapishaji vi tabu nchini.

Wakati mwingi anapozungumza, hadhira hutaka kuendelea kumsikiliza. Wazazi wake na walimu wanamtaja kuwa mwanafunzi mwenye nidhamu na subira. Isitoshe anayo bidii ya mchwa.

“Nafurahi sana kuwa mshindi. Ushindi huu unatokana na bidii, ninamshukuru mungu kuwa utiifu na uaminifu hasa kwa wazazi na walimu hunifaa sana. Hii ni siri ya mafanikio, hakuna siri nyingine,” alisema Zamzam wakati wa mahojiano.

Wakati wa kupokea tuzo hiyo, mwanafunzi huyu aliambatana na walimu wake, viongozi wa kaunti ya lsiolo na mwakilishi wa wanawake katika Kaunti ya lsiolo Lucy Mworia ambaye alisema kuwa eneo mwanafunzi anatoka haku­ wezi kamwe kuwa kizuizi cha kuweza kufanya vyema kwenye masomo, na ukuzaji wa vipaji vyake bora tu mwanafunzi atiwe motisha.

“Wakenya wengi hufikiria kuwa watu wa lsiolo hupenda mifugo pekee lakini sivyo kwa sababu mfano umejitokeza leo waziwazi. Thnafurahia sana kuwa huyu mwana wetu ametutia furaha ambayo hatuwezi kusahau kamwe. Ninataka wanafunzi wengine kutoka lsiolo kuiga, mfano huu,” akasema Bi Mworia.

Mkugenzi wa shule hiyo Bw Macharia anaele­za kuwa hii ilikuwa mara ya kwanza kwa mwa­nafunzi kutoka shule hiyo kupokea tuzo za aina hiyo. Anaongeza kuwa ana hakika kwamba Zamzam atafanya vyema kwenye mtihani wa kitaifa wa KCPE.

eKitabu is East Africa’s premier ebook store. We distribute ebooks and interactive content. Search for ebooks of your choice from www.ekitabu.com . Pay by Mpesa or credit card and read with the free eKitabu App on android smartphone, tablet, laptop or PC.

%d bloggers like this: